Diamond Platnumz - www.wasafi.com

10 Views
Published
Kwanza kabisa ningependa niombe radhi kwa wadau na Mashabiki wote wa muziki kutokana na tatizo fupi liliilojitokeza la mtandao wa wasafi.com kuwa nzito ghafla, na kupelekea ununuzi kuwa slow kutokana na wingi wa wanunuaji... ila ningependa sanasana niwapongeze na kuwashukuru sana sana wadau, Mashabiki na wapenzi wote wa Muziki kwani Mapokezi tulioyaona hatukuyategemea kabisa......kiukweli wakati tunasema tuanzishe wasafi.com tulikuwa na hofu labda wengine hawatasapoti tena kwakuwa nyimbo inatoka kwa kuchangia 300 kwa kudownload na si bure kama ilivyokuwa zamani....ila kiukweli spidi hii ya ununuzi imedhihirisha ni jinsi gani wananchi wanamapenzi ya dhati na wasanii wao, na wako radhi kuwasapoti kwa hali na mali watoto wao wa nyumbani... Nasi tunawashukuru sana na kuwaahidi hatutowaangusha katika utendaji wetu wa kazi... kiukweli wengi elimu yetu ni ndogo na mkombozi ama ajira yetu pekee tunayoitegemea ni mziki walau tupe senti mbili tatu za kununua unga na dagaa ili tuweze kula ugali na na wazazi wetu.... tafadhali tunaomba msiache kutusapoti.... tunafaham kuwa kuna baadhi ya mitandao inachkua nyimbo za wasanii toka wasafi.com na kwenda kuzisambaza bure pasipo makubaliano, ila punde tutawashughurikia ikiwemo kufungiwa mitandao yao, na kupelekwa mahakamani kwa kosa la kuhujumu uchumi kwa kuikosesha mapato TRA...... kutokana na watu kuifollow kwa kasi akaunti yetu ya instagram ya @Wasafidotcom imepelekea instagram waisimamishe kwa muda kwani iliwatia mashaka idadi ya watu waliyoifata kwa mda mfupi... Baada ya masaa mawili mtandao wa www.wasafi.com utakuwa tayari kwa kila mmoja kununua nyimbo ya msanii ampendae na akaunti yetu ya insta punde itakuwa tayari...Shukran
Category
Music
Be the first to comment